Wednesday, October 9, 2019

Emmanuel mayanga
Tel:0757788194


NAOMI OSAKA MJAPANI WA KWANZA KUWAHI KUSHIKA NAMBARI MOJA YA WANAWAKE BORA KATIKA TENIS DUNIANI


Unaweza kumuona akiwa na aibu mbele ya watu mwanadada huyu akiwa na miaka 21 tu akizaliwa huko japan na kwenda kuishi nchino marekani akiwa na miaka mi 3 tu

Sifa yake kubwa ni urembo aibu uwezo wake na akili nyingi pindi anapokua mchezoni

Naomi osaka alizaliwa mnamo october 16 mwaka 1996 wakati naandika makala hii bado siku 8 tu tuione kuelekea birthday au siku yake ya kuzaliwa

Baba yake ni raia wa haiti lakin ana asili ya afrika akiwa mweusi kabisa mama yake ni mjapani ndie mwenye jina la osaka

Baba yake aliamua kutumia jina la mama yake kwa mwanaye ili tu aweze kuthaminiwa na serikali ya marekani inayowabagua watu weusi

Naomi mpaka sasa anakadiriwa kua mwanadada anaye kunja kiasi cha zaidi ya million 11 za marekani katika mchezo huo

Umaarufu wake ulipamba moto kwenye mashindano ya us open baada ya kumtandika serena williums ambaye alikua nguli wa mchezo huo hapo nyuma

Baada ya hapo sasa akashika nafasi ya kwanza kabla ya kushuka hadi nafasi ya 3 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na mwanadada barty wa Australia.

Naomi ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wawili..........kutangaza nasi wasiliana nasi katika namba zainazooonekana hapo juu.